Tuesday, 5 April 2016

KYANYI RESORT HOTEL YAZINDULIWA RASMI LEO HII 28.03.2016 BUKOBA


Padri Faustin Kamuhabwa Baba Paroko wa Parokia ya Bukoba akitoa neno wakati wa Hafra fupi ya Ufunguzi Rasmi wa Hotel ya Kyanyi Resort(kushoto) ni Mkurugenzi wa Hoteli hiyo Dr. Frederick Baijukya. Hoteli hii mpya ipo katika eneo la Kyanyi (Migera B) hatua chache kutoka Bukoba Mjini.
Padri Faustin Kamuhabwa Baba Paroko wa Parokia ya Bukoba akiendesha ibada fupi wakati wa Ufunguzi wa Hoteli


Padri Faustin Kamuhabwa Baba Paroko wa Parokia ya Bukoba akinyunyizia Maji ya Baraka kwenye Maeneo tofauti tofauti ya Hoteli hiyo mpya iliyozinduliwa leo.


Mwonekano wa Kyanyi Hotel kwa mbele







Dr. Frederick Baijukya mmoja wa wahusika na Wamiliki wa Hotel ya Kyanyi Resort akitoa neno kwa Waalikwa (Hawapo pichani) kwenye Eneo la Bustani ya Hotel hiyo yenye Sura mpya Mjini Bukoba. Dr. Frederick amewataka Wafanyabiashara wa Mjini hapa Bukoba kutumia fursa ya Mkoa huu kuwa kitovu cha Biashara kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kujenga kumbi kubwa za mikutano pamoja na hotel mbalimbali.
Dada Stella nae alikuwepo kwenye Uzinduzi wa Hotel hiyo ya Kyanyi Resort
Mmiliki wa Hotel hiyo mpya ya Kyanyi Resort Bi. Pudensiana Rwezaura akitoa neno wakati wa Uzinduzi huo

Dada Stella Daud akiwa na Mtoto Mainda

Wageni waalikwa kwenye Ufunguzi wa Hotel hiyo iliyopo maeneo ya Kyanyi (Migera B) hatua chache kutoka Bukoba Mjini.


Mama PK(kulia) akiwa na Mwanae wakati wa Uzinduzi wa Hotel leo jioni
Mtoto Mainda akiwa kwenye Bustani nzuri ya Hotel hiyo iliyofunguliwa sambamba na Sikukuu ya Pasaka, Hotel ya Kyanyi ipo Eneo la Kyanyi (Migera B) hatua chache kutoka Bukoba Mjini.

Mtoto Mainda alipata picha kwenye Bustani ya Hotel hiyo
Karibu sana...
Muda wa Chakula ulifika

Wakipata Chakula cha usiku

Picha Ilipigwa ya Familia ya Bwana na Bibi Frederick Baijukya
Ngoma ya kihaya nayo ilishika kasi wakati wa Uzinduzi wa Hotel hiyo leo

No comments:

Post a Comment